Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Utumishi wa Mahakama

logo

Welcome note

Prof Ibrahim H. Juma
Prof Ibrahim H. Juma
Mwenyekiti

 

NENO LA UTANGULIZI 

Kwa niaba ya Makamishna, Menejimenti na Watumishi wote wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, ninayo furaha kuwakaribisha wananchi wote kuitembelea Tovuti ya Tume ya Utumishi wa Mahakama iliyoanzishwa kwa lengo la kuuhabarisha Umma kuhusu uwepo wa  shughuli mbalimbali na majukumu yanayofanywa na Tume.

Majukumu ya Tume ya Utumishi wa Mahakama yameainishwa katika Ibara ya 113(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kifungu Na. 29 cha Sheria ya Uendeshaji wa Mahakakama Namba 4 ya mwaka 2011. Majukumu hayo ni Kumshauri Rais kuhusu Uteuzi wa Viongozi wa Mahakama wakiwemo Jaji Kiongozi, Majaji wa Mahakama Kuu Tanzania, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Msajili Mkuu, Msajili wa Mahakama ya Rufani na Msajili wa Mahakama Kuu,

Tume pia inalo jukumu la kumshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya mwenendo wa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kiongozi, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Msajili Mkuu, Msajili wa Mahakama ya Rufani na Msajili wa Mahakama Kuu. Vile vile Tume inamshauri Rais kuhusu maslahi ya watumishi wa Mahakama ya Tanzania.

Vile vile, kusimamia nidhamu na maadili ya Maafisa Mahakama ni moja ya jukumu la msingi la Tume ya Utumishi wa Mahakama. Katika kusimamia maadili, Tume inazo Kamati za Maadili zifuatazo; Kamati ya Maadili ya Majaji, Kamati ya Maadili ya Maafisa Mahakama, Kamati ya Maadili ya Maafisa wa Mahakama ngazi ya Mikoa na Kamati ya Maadili ya Maafisa wa Mahakama ngazi ya Wilaya.

Tume katika kutekeleza majukumu yake ya msingi, inatoa umuhimu

wa pekee kwenye kuimarisha Maadili ya Watumishi wa Mahakama.

Kupitia kamati za Maadili ya Maafisa Mahakama ngazi za Mkoa na Wilaya, Mwananchi anayo nafasi ya kuwasilisha kwa maandishi malalamiko yake yanayohusu ukiukwaji wa maadili miongoni mwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania.

Karibuni sana.

 

Imetolewa na: -

Prof Ibrahim Juma

Mwenyekiti- Tume ya Utumishi wa Mahakama