Majukumu ya Tume

Mamlaka ya Tume ya Utumishi wa Mahakama kama chombo cha kusimamia ajira na nidhamu za watumishi wa Mahakama yanatokana na Ibara 113(1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Toleo la mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Kifungu Na. 29 (1) cha Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4 ya mwaka 2011 nayo ni kama ifuatavyo:

(a)Kumshauri Mhe. Rais kuhusu;

(i)Uteuzi wa Jaji Kiongozi na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania,

(ii)Uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Msajili Mkuu, Msajili wa

Mahakama ya Rufani na Msajili wa Mahakama Kuu,

(iii) Kutokuwa na uwezo kwa Jaji wa Rufani, Jaji Kiongozi au Jaji wa

Mahakama Kuu kutekeleza majukumu ya ofisi,

(iv) Mwenendo usioridhisha wa Jaji wa Rufani, Jaji Kiongozi, MtendajiMkuu wa Mahakama, Msajili Mkuu, Msajili wa Mahakama ya Rufani na Msajili wa Mahakama Kuu,

(v)Maslahi ya watumishi wa Mahakama ya Tanzania.

(b)Kuchambua malalamiko dhidi ya Jaji wa Rufani, Jaji Kiongozi, au Afisayeyote wa Mahakama,

(c)Kuchukua hatua za kiutawala dhidi ya Jaji wa Rufani, Jaji Kiongozi, au Jaji mbali na hatua zilizoainishwa katika Katiba,

(d)Kuteua, kupandisha cheo na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya Maafisa wa Mahakama,

(e)Kuajiri na kupandisha cheo au kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya

mtumishi yeyote ambaye siyo afisa wa Mahakama kama ilivyoainishwa katika sheria.