Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo cha kikatiba kilichopewa jukumu la kusimamia uendeshaji wa Mahakama ya Tanzania. Tume imeundwa na Ibara ya 112 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Kwa mujibu wa Ibara hiyo ya 112 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Tume inaundwa na wajumbe wafuatao;i.    Jaji Mkuu ambaye ni -Mwenyekiti

ii.    Mwanasheria Mkuu wa Serikali- Mjumbe

iii.    Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani ambaye anateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Jaji Mkuu

iv.    Jaji Kiongozi- Mjumbe

v.    Wajumbe wawili ambao wanateuliwa na Rais

Kwa mujibu wa kifungu cha 15 (1) cha Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Na. 4 ya mwaka 2011, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ni Katibu wa Tume na ndiye mtekelezaji wa maamuzi yote ya Tume.   

Aidha, ipo Sekretariet inayoisaidia Tume kwenye utekelezaji wa majukumu yake.

 

Majukumu ya Tume yameainishwa katika Ibara ya 113 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kifungu Na. 29 cha Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Na. 4 ya mwaka 2011 kama ifuatavyo;a)    Kumshauri Rais kuhusui.    Uteuzi wa Jaji Kiongozi na Majaji wa Mahakama Kuu

ii.    Uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Msajili wa Mahakama ya Rufani na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

iii.    Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kiongozi au Jaji wa Mahakama Kuu kushindwa kutekeleza majukumu yake.

iv.    Mwenendo mbaya unaofanywa na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kiongozi, Jaji wa Mahakama Kuu, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Msajili Mkuu, Msajili wa Mahakama Kuu ambao hauendani na maadili ya kazi yake au sheria zinazosimamia maadili ya viongozi wa Umma.

v.    Mishahara na maslahi ya Watumishi wa Mahakama.

b)      Kufanyia uchunguzi malalamiko dhidi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kiongozi au Jaji wa Mahakama Kuu.

c)    Kuchukua hatua za kiutawala dhidi ya Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kiongozi au Jaji ambazo hazikutajwa kwenye Katiba.

d)    Kufanya uteuzi, kuthibitisha, kupandisha cheo na kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wasio Maafisa Mahakama.

e)    Kuajiri, kupandisha cheo, na kuchukua hatua zozote za kinidhamu dhidi ya watumishi wasio Mahakimu.

Tume pia imepewa mamlaka ya Sheria ya kuteua viongozi mbalimbali wa Mahakama wakiwemo Naibu Wasajili na Watendaji wa Mahakama

 

Kifungu cha 33 (1) cha Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Na. 4 ya mwaka 2011, kimeruhusu Tume ya Utumishi wa Mahakama kukasimu utekelezaji wa majukumu yake kwenye Kamati zilizoundwa chini ya Sheria hiyo. Baadhi ya Kamati hizo ni hizi zifuatazo;•    Kamati ya Maadili ya Majaji

•    Kamati ya Maadili ya Maafisa Mahakama

•    Kamati ya Maadili ya Maafisa Mahakama ya Mkoa

•    Kamati ya Maadili ya Maafisa Mahakama ya Wilaya 

(a)    Kamati ya Maadili ya Maafisa Mahakama ya Mkoa inaundwa na wajumbe wafuatao;i.    Mkuu wa Mkoa ambaye ndiye Mwenyekiti

ii.    Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa

iii.    Katibu Tawala wa Mkoa

iv.    Wajumbe wengine wawili wanaoteuliwa na Mkuu wa mkoa kama atakavyoiona kwa kuzingatia kuwa ni watu mashuhuri kwenye mkoa, waadilifu, wenye ufahamu na uwezo unaoistahili kushiriki kikamilifu kufanikisha majukum ya kamativ.    Maafisa wawili wa Mmahakama watakaoteuliwa na Jaji Mfawidhi.vi.    Aidha, Katibu wa Kamati hiyo atakuwa Mwanasheria wa Serikali Mfawidhi katika Mikoa yenye Ofisi ya Mwanansheria Mkuu wa Serikali. Mikoa isiyo na Ofisi hiyo basi Katibu Tawala wa Mkoa atakuwa Katibu wa Kamati.(b)    Kamati ya Maadili ya Maafisa Mahakama ya Wilaya inaundwa na wajumbe wafuatao;i.    Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye Mwenyekiti

ii.    Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya

iii.    Katibu Tawala wa Wilaya-Katibu wa Kamati

iv.    Wajumbe wengine wawili wanaoiteuliwa na Mkuu wa wilaya kama atakavyoona kwa kuzingatia kuwa ni watu mashuhuri, waadilifu, wenye ufahamu na uwezo unaostahili kushiriki kikamilifu kufanikisha majukumu ya Kamati.

v.    Mahakimu wawili wanaoteuliwa na Jaji Mfawidhi.

  

i.    Kupokea malalamiko yanayohusu afisa mahakama yamayohusu mahakimuii.    Kufanya uchunguzi juu ya malalamiko/tuhuma

iii.    Kumwonya Afisa Mahakama juu ya malalamiko dhidi yake kama suala hilo halihitaji kupelekwa mbele ya Tume.

iv.    Kuchukua hatua yoyote ile itakayofaa kulingana na mazingira ama aina ya lalamiko

 

Majukumu ya Kamati za Maadili ya Maafisa Mahakama za Mikoa na Wilaya yanafanana, tofauti iliyopo ni kwamba Kamati ya Mmkoa inashughulika na Mahakimu Wakazi ngazi ya Mkoa na kamati ya wilaya inashughulikia Mahakimu wote walioko kwenye Mahakama za Mwanzo. 

Mtu au Taasisi yeyote inaweza kuwasilisha malalamiko mbele ya Tume au kamati zake iwapo kutakuwepo na ushahidi. Mfano wa 

i.    Afisa Mahakama

ii.    Afisa wa Sheria

iii.    Wakala wa Serikali

iv.    Wakili wa Kujiteggemea

v.    Taasisi ya Serikali

vi.    Mtu yeyote mwenye ushahidi wa kutosha juu ya malalamiko yake.


 

Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Na. 4 ya mwaka 2011 imeeleza kwamba;(a)  Malalamiko yote yanapaswa kuwasilishwa kwa maandishi nay awe na sahihi ya mlalamikaji.(b)  Malalamiko yaswe na taarifa za kutosha kama vile maelezo ya kitendo kilichotendeka na mazingira yake,

Kwa Mfanlo;

Namna kesi ilivyoshughulikiwa

Tuhuma za Rushwa

Kushindwa kutekeleza majukumu

Vitendo vinavyokiuka maadili ya Maafisa Mahakama.


 

Tume imafanya mambo mbalimbali yenye lengo la kuimarisha utendaji kazi wa kamati za Maadili ambayo ni pamoja na;
  • Kutoa mafunzo kwa wajumbe wa kamati

  • Kutoa mwongozo wa uendeshaji wa Kamati

  • Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kuona namna kamati zinavyofanya kazi pamoja na kutoa maelekezo ya kurekebisha kasoro zinazoonekana.

  • Tume kufanya ziara na kukutana na wajumbe wa kamati za Maadili ya Maafisa Mahakama kwa lengo la kuwapa elimu pamoja na kuwakutanisha ili wapate nafasi ya kubadilishana uzoefu.