Kamati hii imeanzishwa chini ya kifungu cha 46 cha Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Sura ya 237. Kamati hii ina jukumu la kushughulikia masuala ya kimaadili dhidi ya Maafisa Mahakama wa ngazi zote ikiwemo Naibu Wasajili isipokuwa Majaji wa Rufani, Jaji Kiongozi na Jaji wa Mahakama Kuu.

Wajumbe

i. Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye ndiye Mwenyekiti.

ii. Majaji wawili wa Mahakama Kuu wanaoteuliwa na Jaji Mkuu

iii. Maafisa Mahakama wawili wanaoteuliwa na Jaji Mkuu wasiokuwa Jaji wa Rufani au Jaji wa Mahakama Kuu.

Aidha, Katibu wa Kamati hii ni Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Majukumu ya Kamati

i. Kupokea malalamiko yanayohusu Afisa Mahakama isipokuwa  Majaji wa Rufani, Jaji Kiongozi au Majaji wa Mahakama Kuu.

ii. Kuwasilisha kwa Afisa Mahakama malalamiko yaliyowasilishwa dhidi yake.

iii. Kuwasilisha malalamiko kwenye Tume

iv. Kuchunguza malalamiko.

v. Kumwonya Afisa Mahakama juu ya malalamiko dhidi yake kama suala hilo halihitaji kupelekwa mbele ya Tume.

vi. Kuchukua hatua yoyote ile itakayofaa kulingana na mazingira.