JAJI MKUU AKUTANA NA WADAU KUIMARISHA UTOAJI WA HUDUMA ZA MAHAKAMA


 Na Mwandishi- Mahakama

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Mhe. George Masaju tarehe 22 Januari, 2026   amekutana na  wadau wa Mahakama kwa lengo la kujadiliana namna ya kuimarisha utoaji wa huduma za Mahakama na Sekta ya Sheria kwa ujumla.

Wadau walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza Johari, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Eliakim Maswi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Antony Sanga, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo, Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Bi. Bibiana Kileo na Wadau wengine. 

Kikao hicho kilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaji Mkuu Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. 

Aidha, Kwa upande wa Mahakama kikao hicho kilihudhuriwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya, Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. George Herbert, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri, Mhe. Desdery Kamugisha, Mkurugenzi wa Maktaba, Mhe. Kifungu Kariho na Maafisa wengine wa Mahakama.