Kamati ya Nidhamu ya Makao Makuu inahusika na uchunguzi wa tuhuma za ukiukwaji wa maadili dhidi ya watumishi wasiokuwa maafisa mahakama katika Makao Makuu na Mahakama ya Rufani.

Wajumbe wa Kamati.

Kamati ya Nidhamu Makao Makuu na Mahakama ya Rufani inaundwa na:

i. Mwenyekiti atakuwa Mtendaji wa Mahakama ya Rufani;
ii. Mkuu wa Idara atakayeteuliwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama;
iii. Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu atakuwa Katibu;
iv. Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani;
v.  Afisa mwandamizi mtaalamu kwenye eneo husika aliependekezwa na mtendaji mkuu wa mahakama;

Majukumu ya Kamati.

i. Kufanya uchunguzi wa awali ili kubaini ukweli wa kosa ambalo mfanyakazi anadaiwa kulifanya;

ii. Pale inapohitajika, kutoa adhabu au kuchukuwa hatua dhidi ya mtumishi kama ilivyoainishwa katika kanuni;Kuunda kamati ya uchunguzi itakayojumuisha si chini ya wajumbe wawili na si zaidi ya wanne, ambao hawatakua watumishi wa Mahakama, Kamati itajumuisha mjumbe mwanaume na mwanawake;

iii. Kutoa adhabu kama ilivyoainishwa katika Sehemu B ya Jedwali la Pili la Kanuni baada ya kamati ya uchunguzi kuwasilisha ripoti yake na kubaini kuwa kosa hilo halistahili kusababisha mtumishi kufukuzwa kazi, kupunguzwa mshahara au cheo.