Kamati ya Maadili ya Maafisa Mahakama ya Wilaya inashughulikia malalamiko dhidi ya Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo. Kamati hizi zimeundwa chini ya kifungu cha 51 cha Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Sura ya 237.
Wajumbe
i. Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati.
ii. Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya.
iii. Katibu Tawala wa wilaya (DAS) ambaye ndiye Katibu wa Kamati.
iv. Wajumbe wawili wanaoteuliwa na Mkuu wa Wilaya, miongoni mwa watu mashuhuri, waadilifu, wenye ufahamu na uwezo unaostahili kushiriki kikamilifu kufanikisha majukumu ya kamati ya mahakama ya Wilaya. Mjumbe mmoja kati yao anapaswa kuwa kiongozi wa dini.
v. Maafisa Mahakama wawili wanaoteuliwa na Jaji Mfawidhi.
Majukumu ya Kamati
i. Kupokea na kupeleleza malalamiko yaliyowasilishwa na wananchi dhidi ya Mahakimu wa Mahakama ya Mwanzo waliopo katika Wilaya husika na kuwasilisha ripoti Tume.
ii. Kufanya uchunguzi wa mwenendo wa Mahakimu wa Mahakama ya Mwanzo kwa kuzingatia maelekezo ya Jaji Mfawidhi na kuripoti kwake.