Kamati ya Maadili ya Majaji imeanzishwa chini ya kifungu cha 37 (1) cha Sheria ya Usimamizi wa Mahakama sura ya 237. Kamati hii inalo jukumu la kusimamia maadili ya Majaji.  

Wajumbe

Kamati hii inaundwa na wajumbe wafuatao;

i. Mwenyekiti wa Kamati hii ni Jaji wa Mahakama ya Rufani anayeteuliwa na Jaji Mkuu.

ii. Wajumbe wengine wa Kamati hii ni Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani wanaoteuliwa na Jaji Mkuu; na

iii. Majaji watatu wa Mahakama Kuu wanaoteuliwa na Jaji Mkuu.

Aidha, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania ndiye Katibu wa kamati hii.

Majukumu ya Kamati

i. Kupokea na kupeleleza malalamiko dhidi ya Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kiongozi au Jaji wa Mahakama Kuu.

ii. Kuwasilisha kwa Jaji wa Rufani, Jaji Kiongozi, au Jaji wa Mahakama Kuu malalamiko yaliyowasilishwa dhidi yake.

iii. Kuwasilisha malalamiko kwenye Tume

iv. Kusikiliza malalamiko dhidi ya Jaji.

v. Kumuonya Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kiongozi au Jaji wa Mahakama Kuu kuhusiana na malalamiko yanayomhusu kama malalamiko hayo hayastahili kuwasilishwa kwenye Tume.

vi. Kuchukua hatua nyingine yoyote ile kama itakavyoonekana inafaa kulingana na mazingira.