WANAWAKE TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA WASHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.


WANAWAKE TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA WASHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

Watumishi Wanawake wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wameungana na wanawake wengine Duniani kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani.

Siku hii ni Maalumu ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi kwa lengo la kutambua mchango wa wanawake katika maendeleo ya jamii, uchumi na uongozi.

Katika maadhimisho hayo, watumishi hao walipata fursa ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uwezeshaji wa wanawake mahali pa kazi, usawa wa kijinsia, pamoja na umuhimu wa kuendelea kujenga uwezo wa wanawake ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa majukumu yao.

Aidha, maadhimisho hayo yalisisitiza umuhimu wa mshikamano miongoni mwa wanawake, kuhamasishana katika kujitambua na kutumia ipasavyo fursa za Watumishi zilizopo ili kuleta maendeleo binafsi na ya Taasisi kwa ujumla.

Tume ya Utumishi wa Mahakama imeendelea kuthamini mchango wa wanawake katika utumishi wa umma kwa kuhamasisha mazingira ya kazi yenye usawa, kuheshimu haki na kutoa fursa sawa za maendeleo kwa watumishi wote.
Kaulimbiu ya mwaku huu ni “ Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana. Msingi Jumuishi kufikia Dira 2050.” Hii ni kaulimbiu inayosisitiza umuhimu wa kuhakikisha wanawake na wasichana wanapata haki na fursa sawa katika nyanja zote za maendeleo.