Kamati ya Nidhamu ya Masjala Kuu ya Mahakama Kuu inahusika na uchunguzi wa tuhuma za ukiukwaji wa maadili dhidi ya watumishi wasiokuwa Maafisa Mahakama katika Masjala Kuu ya Mahakama Kuu.

Wajumbe wa Kamati.

Kamati ya Nidhamu ya Masjala Kuu ya Mahakama Kuu inaundwa na:

i. Mtendaji wa Mahakama kuu ambaye atakuwa mweyekiti;

ii. Mtendaji wa mahakama anayehusika na Mahakama Kuu ambaye atakuwa katibu;

iii. Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu;

iv. Mkuu wa idara aliyeteuliwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama asiyekuwa afisa rasilimali watu au afisa mahakama; na

v. Afisa mwandamizi kutoka idara za kitaalamu alieteuliwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama.

Majukumu ya Kamati.

i. Kufanya uchunguzi wa awali ili kubaini ukweli wa kosa ambalo mfanyakazi anadaiwa kulifanya;

ii. Pale inapohitajika kutoa adhabu au kuchukuwa hatua dhidi ya mtumishi kama ilivyoainishwa katika kanuni;Kuunda kamati ya uchunguzi itakayojumuisha si chini ya wajumbe wawili na si zaidi ya wanne, ambao hawatakua watumishi wa Mahakama, Kamati itajumuisha mjumbe mwanaume na mwanawake;

iii. Kutoa adhabu kama ilivyoainishwa katika Sehemu B ya Jedwali la Pili la Kanuni baada ya kamati ya uchunguzi kuwasilisha ripoti yake na kubaini kuwa kosa hilo halistahili kusababisha mtumishi kufukuzwa kazi, kupunguzwa mshahara au cheo.