Wadau wetu ni yeyote anayenufaika na huduma zetu za ajira, teuzi na uwasilishaji wa malalamiko yanayohusiana na ukiukwaji wa maadili ya watumishi wa Mahakama. Wanufaika hawa wanaweza kuwa taasisi za umma au binafsi, mwananchi yeyote mwenye sifa za kuajiriwa kwa nafasi zilizotangazwa na Tume na mtu au taasisi yenye maslahi au ushahidi katika lalamiko la ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa Mahakama lililowasilishwa.