Kamati ya Nidhamu ya Kanda na Divisheni za Mahakama Kuu ya Tanzania inashughulikia masuala ya nidhamu kuhusu watumishi wasiokuwa Maafisa Mahakama katika Kanda na Divisheni za Mahakama Kuu ya Tanzania.
Wajumbe wa Kamati.
Kamati ya Nidhamu ya Kanda au Divisheni ya Mahakama Kuu inaundwa na:
i. Katibu tawala msaidizi wa (utawala na rasilimali watu) kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa au katibu tawala wa wilaya au mkurugenzi wa rasilimali watu kutoka taasisi ya umma inayotambulika ambaye atakuwa mwenyekiti;
ii. Naibu msajili Mahakama Kuu wa Kanda au Divisheni;
iii. Mtendaji wa mahakama wa kanda au divisheni ya mahakama kuu ambaye atakuwa katibu;
iv. Mjumbe aliyeteuliwa na Jaji Mfawidhi asie afisa rasilimali watu au afisa mahakama; na
v. Afisa mwandamizi kutoka idara za kitaalamu aliyeteuliwa na Jaji Mfawidhi.
Majukumu ya Kamati.
i. Kufanya uchunguzi wa awali ili kubaini ukweli wa kosa ambalo mfanyakazi anadaiwa kulifanya;
ii. Pale inavyohitajika, kutoa adhabu au kuchukuwa hatua dhidi ya mtumishi kama ilivyoainishwa katika kanuni;Kuunda kamati ya uchunguzi itakayojumuisha si chini ya wajumbe wawili na si zaidi ya wanne, ambao hawatakua watumishi wa Mahakama, Kamati itajumuisha mjumbe mwanaume na mwanawake;
iii. Kutoa adhabu kama ilivyoainishwa katika Sehemu B ya Jedwali la Pili la Kanuni baada ya kamati ya uchunguzi kuwasilisha ripoti yake na kubaini kuwa kosa hilo halistahili kusababisha mtumishi kufukuzwa kazi, kupunguzwa mshahara au cheo.