Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amuapisha Jaji Siyani Kuwa Jaji Kiongozi Wa Mahakama Kuu Ya Tanzania


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji Mustapher Siyani kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Jaji Siyani anachukua nafasi ya Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi aliyekuwa Jaji Kiongozi ambaye ameteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kabla ya uteuzi huo Jaji Siyani alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.Kwa mjibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na sharia namba 4 ya uendeshaji wa Mhakama Jaji Kiongozi anatambulika kama mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama hivyo Jaji Siyani atakuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.