TUME YAJIKITA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUBORESHA HUDUMA ZA MAHAKAMA


Na Lydia Churi- Tume ya Utumishi wa Mahakama

Tume ya Utumishi wa Mahakama itatekeleza ipasavyo jukumu lake la kusimamia maadili ya watumishi wa Mahakama ya Tanzania ili huduma zinazotolewa na Mhimili huo ziwe bora na ziendane na maboresho ya huduma yanayoendelea hususan miundombinu ya majengo na Tehama.

Naibu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama (Ajira n a Uteuzi) Bibi Enziel Mtei aliyasema hayo jana wakati wa mkutano wa hadhara katika kata ya Magoweka wilaya ya Gairo mkoani Morogoro uliolenga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uwepo wa Tume hiyo ambayo moja ya majukumu yake ni kupokea na kushughulikia malalamiko ya wananchi yanayohusiana na ukiukwaji wa maadili kwa Maafisa Mahakama.

Alisema kwa kuwa Tume ya Utumishi wa Mahakama ni mamlaka ya nidhamu ya watumishi wa Mahakama inaona kuwa hata yakijengwa majengo mazuri na kuwa na mifumo mizuri au tukiajiri watumishi wengi, kama watumishi hawatakuwa na maadili bado wananchi itakua ni kero”, alisema.

Alisema Tume imeamua kujikita kwenye suala la kusimamia maadili ya watumishi ili ubora wa huduma zinazotolewa uendane na majengo mazuri yanayojengwa na Mahakama ya Tanzania pamoja na mifumo ya”Tume itaendelea kumchukulia hatua za kinidhamu mtumishi yeyote atakayekiuka maadili kwa kuwa ni jukumu lake na hakuna mtu aliye juu ya sheria, alisema” Naibu Katibu huyo.

”Tume itaendelea kumchukulia hatua za kinidhamu mtumishi yeyote atakayekiuka maadili kwa kuwa ni jukumu lake na hakuna mtu aliye juu ya sheria, alisema Naibu Katibu huyo.

Alisema Tume ya Utumishi wa Mahakama imeweka mifumo ya kusimamia maadili ya Maafisa Mahakama hivyo aliwomba wananchi kuwa na imani na Tume na kwamba mtu yeyote mwenye malalamiko asisite kuwasilisha mahali panapohusika.

Awali akitoa Mada kuhusu uwepo wa Kamati za Maadili ya Maafisa Mahakama na majukumu yake, Naibu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama (Nidhamu na Maadili) Bi. Alesia Mbuya alisema zipo kamati zinazoshughulikia maadili ya Maafisa Mahakama kuanzia Majaji, Mahakimu pamoja na watumishi wengine wa Mahakama.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Gairo ambaye pia ni Mwenyeki wa Kamati ya Maadili ya Maafisa Mahakama ngazi ya Wilaya, Jabir Omar Makame aliwataka wananchi wa Wilaya ya Gairo wenye malalamiko yanayohusiana na maadili ya Maafisa Mahakama kuwasilisha kwenye kamati yake ili yashughulikiwe.

”Kamati hizi ndiyo sehemu sahihi ya kuwasilisha malalamiko, tumejipanga kupita kila Kata na kila Kijiji kutoa elimu, pia kila ninapofanya mikutano na wananchi vijijini nitaongeza ajenda ya uwepo wa Kamati za Maadiliya Maafisa Mahakama ili wanachi wazifahamu na kuzitumia”, alisema.

Tume ya Utumishi wa Mahakama imeweka mkakati wa kuwafikia wananchi moja kwa moja na kutoa elimu kuhusu uwepo wa kamati zinazopokea malalamiko ya ukiukwaji wa maadili kwa Maafisa Mahakama na namna ya kuwasilisha malalamiko hayo. Katika awamu ya kwanza Tume inatoa