TUME YAENDELEA KUTOA ELIMU KWENYE MAONESHO YA SABASABA
Tume ya Utumishi wa Mahakama inaendelea kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali wanaotembelea Maonesho ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika jijini Dar es salaam
Aidha, Tume inawakaribisha wananchi wote kutembelea Banda lake lililopo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es salaam ndani ya Banda la Mahakama ya Tanzania.
Ndani ya Banda la Tume, wananchi watapata fursa nzuri ya kufahamu uwepo wa Tume, Majukumu yake na faida zake kwa wananchi.