RAIS SAMIA AMEMTEUA TENA MHE. HAMZA JOHARI KUWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
RAIS SAMIA AMEMTEUA TENA MHE. HAMZA JOHARI KUWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 03 Novemba, 2025 amemteua Mhe. Hamza Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kwa mujibu wa Ibara ya 112(1)(b), Mwanasheria Mkuu wa Serikali atakuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kati ya Wajumbe Sita.
Aidha, taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi imesema kuwa Mhe. Johari ataapishwa kesho tarehe 5 Novemba, 2025 saa nne Asubuhi, Ikulu Chamwino, jijini Dodoma

