RAIS SAMIA AMUAPISHA MHE. HAMZA JOHARI KUWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI.


RAIS SAMIA AMUAPISHA MHE. HAMZA JOHARI KUWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuapisha Mhe. Hamza Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo tarehe 05 Novemba, 2025 Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa kifungu cha 112 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Hamza Johari atakuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Rais Samia tarehe 03 Novemba, 2025 alimteua Mhe. Hamza Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Aidha hafla hiyo imehudhuriwa na wageni mbalimbali ikiwemo Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Akson, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. George Mcheche Masaju, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Wakuu wa Taasisi, Wakuu wa Ulinzi na Usalama, Makatibu na Manaibu Katibu