Raisi ateuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Dkt. Feleshi anachukua nafasi ya Prof. Adelardus Kilangi aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Feleshi alikuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na pia alikua mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.Kwa mjibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na sharia namba 4 ya uendeshaji wa Mhakama mwanasheria Mkuu wa serikali anatambulika kama mjumbe wa Tume hivyo Dkt. Feleshi ataendelea kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.